Sambaza....

Umewahi fikiria kama orodha ya wafungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara ingekuwa haina wachezaji wa kigeni?  Hivi karibuni kumekuwa na mchakato wa kuangalia orodha ya wachezaji wa kigeni katika ligi kuu yetu. Lengo ni kupunguza idadi ya wachezaji hao katika klabu zetu.

Kahata na Kagere wakishangilia moja ya bao.

Na.MchezajiTimuNafasi
1rwaMeddie KagereMshambuliaji226
2tanWaziri JuniorMshambuliaji130
3tanReliants LusajoMshambuliaji120
4tanPeter MapundaKiungo122
5zamObrey C. ChirwaMshambuliaji120
6tanYussuf MhiluMshambuliaji121
7codDavid MolingaMshambuliaji111
8tanDarueshi Saliboko sefuMshambuliaji111
9tanPaulo NongaMshambuliaji100
10bdiBigirimana BlaiseMshambuliaji100

Hebu tujadili kwa pamoja baada ya kuangalia msimamo huu wa wafungaji. Iwapo si Meddie Kagere, Simba SC, mwenye magoli 19 baada ya ligi kusimama, basi mfungaji bora angekuwa na magoli 11 hadi sasa. Ukiangalia pia wachezaji hao ambao wanakimbizana kuchukua kiatu cha ufungaji kwa wachezaji wa ndani, hawana ‘consistent’ katika ufungaji magoli.  Kagere anaweza kwenda likizo mechi mbili au moja, lakini kuna wachezaji wanaweza kwenda likizo hata mechi tano hadi sita.

Swali kuu, je Safu yetu ya Watanzania katika Kupachika mabao ipo dhaifu au haijajifunza bado kwa Okwi na Meddie Kagere? Mshambuliaji tunayemtegemea timu ya taifa anayecheza Ligi Kuu Tanzania Bara anagoli ngapi?

Sambaza....