Jerry Murro msemaji wa zamani wa Yanga sc ameendelea kutoa ya moyoni katika mahojiano katika redio ya Wasafi fm safari hii akiongelea uwezo wa mwalimu mpya wa Yanga Luc Eymaell raia wa Ubeligiji.
Jerry Murro amesema ni afadhali timu angepewa mzawa Mkwasa kuliko Luc na hii ni kutokana na timu kuhitaji matokeo na si kutengeneza timu.
Jerry Murro “Ni vyema tungempa timu Mkwassa lakini sio huyu mzungu, uwezo wa wa Mkwasa ni mkubwa kuliko Luc. Tazama timu inavyocheza haitupi matokeo.
Mwalimu ameshindwa kuinua viwango vya wachezaji hata kama wachezaji ni wabovu. Tunategemea mwalimu ainue viwango vya wachezaji waliopo chini wacheze vizuri na wachezaji wanaocheza vizuri wacheze vizuri zaidi. Lakini imekua tofauti.”
Jerry Murro pia ameuelezea uwezo wa Mkwasa huku akiamini katika mbinu za mzawa huyo.
Murro “Namjua Mkwasa vizuri nilikua nae kipindi kile akiwa na babu Hans na tumeona alivyokua na timu kwa muda timu ilikua vizuri. Ni afadhali mara mia timu akapewa Mkwasa lakini sio huyu Mzungu. Timu inahitaji matokeo na si kusubiri”.