Jana Yanga walitoa sare nyingine ya nne mfululizo dhidi ya Coastal Union katika uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga . Sare ambayo imewaweka katika mazingira magumu ya kufukuzia ubingwa wa Tanzania Bara .
Yanga mpaka sasa hivi wako nyuma ya alama 21 dhidi ya mabingwa watetezi Simba ambao ndiyo wanaoongoza msimamo wa ligi kuu Tanzania bara .
Kuwa nyuma ya alama 21 inaonekana kama mtihani mkubwa kwa Yanga kupata ubingwa wa ligi kuu tena . Mtandao huu ulimtafuta Afisa Habari wa klabu hiyo Hassan Bumbuli.
Mtandao huu ulimtafuta Hassan Bumbuli kujua kama wamekata tamaa na matokeo haya , Hassan Bumbuli amedai kuwa hawajaka tamaa kwa sababu ya sare wanazozipata .
“Hatujakata tamaa , kupata sare ni kawaida sema hizi sare zimekuja mfululizo sana . Ila kupata sare ni kitu cha kawaida hata msimu uliopita tulipata sare”- alisema Hassan Bumbuli.
“Hizi sare hatukuzitegemea , ila hatukaja tamaa bado ligi ina mechi 16 ili iishe kwa hiyo ni mechi nyingi sana ambazo zinaweza zikatufanya tuwe mabingwa”- alimalizia Hassan Bumbuli.