Sambaza....

Klabu ya Coastal Union imefanikiwa kufanikisha ndoto za mshabuliaji wake Muhsin Makame baada ya kufanikisha usajili wake  Barani Ulaya.

Muhsini Makame aliekua akikitumikia kikosi cha “Wagosi wa Kaya” katika eneo la ushambuliaji amefanikiwa kujiunga na Crvena Zvezda ya nchini Serbia baada ya kufuzu majaribio aliyoyafanya kwa mwezi mmoja nchini humo.

Muhsin ambae pia amekitumikia kikosi cha Serengeti Boys kwa sasa ana miaka 19. Baada ya kufuzi majaribio yake amepelekwa katika kikosi cha pili cha timu hiyo ili aweze kukuzwa na kutumika hapo baadae.

Muhsin Makame akiwa katika klabu yake mpya!

 

Mpaka sasa Muhsin Makame ameshiriki katika Ligi ya vijana ya U20 akiwa na Zvezda huku akiwa amecheza mechi 9 na kufunga mabao matano.

Crvena Zvezda inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Serbia ambayo inayoshirikisha jumla ya timu 16 inashika usukani wa ligi hiyo ikiwa na alama 55 katika michezo 20.

Timu hiyo imekua na rekodi nzuri katika Ligi ya kwao huku msimu ikishiriki Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya. Timu hiyo ilikua kundi B pamoja na vigogo Bayern Munich na Totenham Hotspurs.

Muhsin Makame akiwa katika moja ya mechi za U20 nchini Serbia.

Wababe hao wa Serbia wanatumia uwanja wa Stadion Rajko ambao una uwezo wa kubeba watazamaji 51,800 huku klabu hiyo ikiwa imeanzishwa mwaka 1945.

Muhsin Makame ameiacha klabu yake ya Coastal Union ikiwa katika nafasi nzuri katika msimamo wa VPL, huku pia uongozi wa wa Wagosi hao wakionekana kufurahia hatua ya kijana wao huyo ambae amepitia katika timu yao ya vijana.

Sambaza....