Sambaza....

Dakika 45 za kipindi cha kwanza zilikuwa dakika nzuri sana kwa Polisi Tanzania . Dakika ambazo ziliwapa nguvu ya kuongoza kwa goli moja kwa bila huku wakikosa nafasi nyingi za wazi.

Kipi kilipawa nguvu Polisi Tanzania katika mchezo wa jana ? Kuna vitu viwili ambavyo vilikuwa vimewapa nafasi kubwa ya kutawala ule mchezo hasa hasa kipindi cha kwanza.

Wakati Simba walipokuwa na mpira , Polisi Tanzania walijaribu kufanya hard pressing . Hii iliwanyima uhuru Simba kutokuwa huru kipindi walipokuwa na mpira ndiyo maana Polisi Tanzania walikuwa wana pokonya mipira na kuanzisha mashambulizi.

Kitu cha pili , wakati Polisi Tanzania ilipokuwa ina mpira, wachezaji wa Simba walikuwa hawafanyi hard pressing. Walikuwa wanawapa uhuru wachezaji wa Polisi Tanzania walipokuwa na mpira.

Double Pivot Kati ya Greson Fraga na Sharaf Shibob haikufanya vizuri. Kwa sababu Sharaf Shibob hakuwa na ufasaha kipindi alipohitajika kushuka chini kukaba , mara nyingi Sharaf Shibob hucheza vizuri akiwa juu zaidi kuliko kucheza katikati ya mabeki na viungo wa Kati.

Gerson Fraga akishangilia baada ya kufunga goli.

Kipi kilibadilika? baada ya Ibrahim Ajib kuingia , Chama alirudi kucheza kama kiungo wa juu na Greson Fraga , Greson Fraga alikuwa anacheza chini , hakuwa na uwezo wa yeye kusogea tena mbele kama mwanzo alipokuwa anacheza na Sharaf Shibob.

Ibrahim Ajib aliongeza kasi kwa mabeki wa Polisi Tanzania, pia anaongeza ubunifu ambao awali haukuwepo kabisa kwa upande wa Simba . Akawezesha kutoa pasi ya mwisho ya goli pamoja na kufunga goli. Hakuwa na Madoido kama ya Bernard Morrison, Ila alihakikisha anafanya mabadiliko kwenye mchezo.

Sambaza....