Sambaza....

Kocha Mkuu wa Kilimanajaro Stars Juma Mgunda leo ametaja kikosi cha wachezaji 22 watakaounda kikosi cha Tanzania Bara kinachokwenda kushiriki michuano ya Challenge nchini Uganda.
Juma Mgunda katika kikosi chake amemuacha nahodha wa KMC na kipa mkongwe Juma Kaseja ambae amekua mlinda mlango namba moja wa kocha Ettiene Ndayiragije tangu akabidhiwe timu ya Taifa.

Kikosi kamili cha wachezaji 22 wanaondoka ni, Metacha Mnata (Yanga), Aishi Manura (Simba), David Kisu (Gor Mahia), Juma Abdul (Yanga), Nickson Kibabage (Difaa El Jadida), Gadiel Michael (Simba), Mwaita Gereza ( Kagera), Mohamed Hussein (Simba), Kelevin Yondani (Yanga), Bakari Mwamnyeto (Coastal Union) na Baraka Majogoro (Polisi Tanzania).
Wengine, Jonas Mkude, Mzamiru Yassin, Hassan Dilunga (wote Simba), Zawadi Mauya (Kagera), Ditram Nchimbi (Polisi Tanzania), Mkandala Cleoface (Prisons), Miraji Athuman (Simba), Eliuter Mpepo (Buildcon-Zambia), Lukasi Kikoti (Namungo) na Rashid Chombo (IK Frej Taby- Sweden)

Sambaza....