Baada ya Jana Simba kufanikiwa kutoka na ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika uwanja wa Uhuru, Afisa Habari wa Ruvu Shooting , Masau Bwire amedai Simba ilikuwa ni mzigo mzito uliozamisha meli.
“Leo mzigo ulikuwa mzito sana umezamisha meli. Pamoja na kwamba mzigo ulikuwa mzito , kwa walioangalia mechi tumefungwa kiajabu ajabu. Angalia magoli yote tuliyofungwa yameingia kwa bahati”.
“Angalia goli la kona na magoli mengine sijui yalikuwa yanapitaje mpaka unajiuliza golini kulikuwa na nini mpaka magoli yalikuwa yanapita vile. Nilikuwa nimekaa kule juu nikawa najiuliza haya magoli yanaingiaje”.
“Pamoja na kufungwa Simba ni timu ya kawaida sana. Kwa mtu anayejua mpira ameona tulivyocheza mpira, Simba ni timu ya kawaida. Tutakutana nao kwenye mzunguko wa pili tutahakikisha mzigo hautokuwa mzito tena”. Alisema Afisa Habari huyo mwenye maneno mengi. Kwa matokeo hayo Simba imejikita kileleni mwa maimamo wa ligi kuu.