- Safari ya Yanga, Mikononi mwa Dube
- Simba na Yanga nani anaongoza kuweka mpira kwapani.
- Yanga Waweweseka! Gamondi Nje!
- Fadlu Tunaamini anawapa Ubingwa Wekundu
- Manuel Neuer ana umri sawa na uchambuzi wa soka kwa kompyuta
Matokeo ya Yanga na Zesco hakika hayakutarajiwa na mashabiki wengi wa timu hiyo. Wengi waliwekeza akili zao kwenye ushindi mnono wa bao juu ya mbili, japo wengi walitarajia zaidi kwenye magoli matatu. Lakini ni makumi 9 ndiyo yaliyoshindwa kuwapa Yanga goli tatu mjue wapwa!
Kwa rika langu na juu yangu wengi wetu watakumbuka walimu wazamani mashuleni kwetu walivyofundisha hasa madarasa ya awali kuhusu makumi, katika hisabati. Hivyo mtu akikwambia makumi tisa (9), hii ina maana ni 90. Katika mpira makumi 9 ni dakika 90 wapwa, nawapa hili angalizo mapema msije zima radio hapa hahaa…haya tuendelee mpwa.
Walioweka sheria za mchezo wa mpira wa miguu waliipa hii kama sheria namba saba (no 7) ya muda wamchezo (time duration) ambapo inasema ni dakika 90 mchezo wa kawaida, lakini yumkini ikawa ni kwa mechi ya mtoano au inayohitaji maamuzi ya kusonga mbele au kuhitimisha jambo( final) basi dakika 120 zitahusika.
Wapwa, kama wewe ni mdau wasoka na unakaa vijiwe mbalimbali vya soka aka kandanda, Mashabiki wa Yanga walikuwa wanazungumza kwenye ushindi wa bao 3 wakitumia neno “uwanja wanyumbani”. Kila utakaye muuliza unasababu gani ya kupata huo ushindi wa 3 sifuri “Majibu tunacheza nyumbani”.
Pamoja na kutokupata hizo bao 3, nini kiliwasibu Yanga kutofanikiwa kupata mabao hayo matatu au mengi katika mchezo huo?
Kiufundi timu ya Yanga inamatatizo makubwa kwenye umaliziaji. Wapo wanaogusa washambuliaji wabovu au hamna washambuliaji kiukweli. Wapwa zangu niwashike sikio kwa nguvu, jukumu la kufunga katika football ya kisasa si lawashambulia tu. Ukumbuke na utambue kuwa yeyote aliyemchezoni anapaswa na kuifungia timu kama mazingira yatamruhusu.
Kwa Yanga iliyocheza na Zesco ilitengeneza nafasi nyingi Sana lakini walikuwa wanazielekezea kwa washambuliaji wawili tu kana kwamba ndio wanawajibu wa kufunga ambaye ni Sibomana na Sadney. Hata wale wachache ambao walipata nafasi za kufunga kama Mapinduzi Balama na Tshitshimbi bado walighafirika kufanya maamuzi ya kufunga wakitafuta mtu wa kumpasia, wanapo rudi kufikiri kufunga mianya imeshazibwa tayari.
Jukumu la kufunga kwenye timu ni la wote waliopo mchezoni, japo timu inaweza kumuandaa mfungaji. Lakini ndani ya mchezo mkasoma kitu toka kwa mfungaji wenu harafu timu ikabadilika kimbinu maana yake ikajua kuwa leo mfungaji wetu hayupo mchezoni na ndipo hapa walipopaswa kubadili uelekeo wa mipira kwenda kwa Sadney.
Hapa ndio unapopata utofauti wa Zesco na Yanga katika mechi hii, ZESCO washambuliaji wao hawajihusishi kwenye ‘move’ ila ‘wanajipossition’ kwenye eneo zuri kuweza kufunga. Mfano ‘angle c’ lile eneo la D ya kwenye 18 ambapo hata Kamusoko alikuwepo na kuweza kufunga.
Eneo jingine lilioonesha udhaifu ni idara ya kiungo ambayo walikuwa wachezaji wanne vijana wenye nguvu (aggressive) Fei Toto, Makame ,Mo banka na Tshitshimbi lakini walishindwa kuwahimili viungo kama Kamusoko, Kasumba, Amaru na kuwaacha watakate.
Jukumu la Yanga kwa wakati huu ni nini.
Bench la ufundi linahitaji kapata mbinu za ufungaji kwa wachezaji wote wanaopata nafasi kucheza. Haiwezekani timu itengeneze nafasi za wazi juu ya tano bila kufunga, na kuja kupata goli la mpira uliokufa ambao ni penati.
Wapa tukubaliane kuna kitu kinakosekana Yanga kwenye pettern yao ya kucheza hasa umaliziaji. Game ya Zambia haijaisha pamoja na ukweli majaliwa ya Yanga kwenye kusonga mbele ni majaliwa ya nyota ya Jaha. Ila Yanga ana jukumu zito zaidi kuliko game ya kwanza, kwa kile kilichoonekana kwa ZESCO wanauwezekano mkubwa kupata goli nyumbani. Kitu ambacho kitalazimisha Yanga nao kupata goli.
Je ndani ya kikosi cha Yanga na wachezaji wake wanaweza kutumia ufinyu wa nafasi moja (Golden opportunity ) kama ya Kamusoko kuamua game hasa kama nafasi juu ya tano hawakuweza kufunga?. Tusihukumu sana kwa kuwa huu ni mchezo wa mpira wa miguu lolote linaweza kutokea.
Lakini Makumi 9 ya hapa nyumbani yangegawika kwa 30 tugeona magoli matatu Leo Yanga Angekuwa na zaidi ya 75% kufuzu makundi Kabla ya mchezo wa marudiano.