Mshambuliaji wa Real Madrid, Mbelgiji Edin Hazard ameanza rasmi leo katika mchezo wa ligi kuu nchini Hispania dhidi ya Levante ikiwa ameshazikosa mechi tatu za mwanzo.
- Safari ya Yanga, Mikononi mwa Dube
- Simba na Yanga nani anaongoza kuweka mpira kwapani.
- Yanga Waweweseka! Gamondi Nje!
- Fadlu Tunaamini anawapa Ubingwa Wekundu
- Manuel Neuer ana umri sawa na uchambuzi wa soka kwa kompyuta
Katika mchezo huo, Hazard alionekana kupata nafasi ya hata kuandika goli lake la kwanza lakini alishindwa kutumia nafasi ipasavyo. Ikumbukwe Hazard ametoka kusumbuliwa na majeraha ya paja kiasi cha kumfanya kushindwa kuanza mechi 3 za awali.
Kwa upande wake mchezaji huyo amesema kuwa ni mwanzo mzuri kwake, kwa kuwa ilikuwa ni ndoto yake kuchezea klabu kama Real Madrid.
“nina furaha kwa sababu naweza kucheza na hata kupata ushindi.. ukitoka majeruhi ni vigumu sana kuwa na kasi yako iliyoizoeleka lakini kikubwa kwangu ni ushindi tulioupata” alisema Hazard.
Madrid wameibuka na ushindi wa goli 3-2 dhidi ya Levante magoli yamewekwa kambani na Karim Benzema mawili na Casemiro katika kipindi cha kwanza huku ya Levante yakifungwa na Borja Mayoral na Gonzalo Melero katika dakika ya 49 na 75 mtawalia.
Kwa matokeo hayo kwa sasa, Real inajikuta ipo
katika nafasi ya pili katika msimamo wa La Liga ikiwa na alama 8 ikicheza mechi
4 nyuma ya Atletico Madrid wenye alama 9
katika nafasi ya kwanza wakicheza michezo minne.