Kocha wa Majogoo wa Jiji Liverpool, Jurgen Klopp amekiri kuwa ni vigumu kwake kuvaa suti katika mechi za timu yake. Akielezea kuhusu kutoonekana kama makocha wengine, Klopp amesema kuwa ni vigumu sana kwa yeye kupumua vyema akiwa amevalia suti.
- Safari ya Yanga, Mikononi mwa Dube
- Simba na Yanga nani anaongoza kuweka mpira kwapani.
- Yanga Waweweseka! Gamondi Nje!
- Fadlu Tunaamini anawapa Ubingwa Wekundu
- Manuel Neuer ana umri sawa na uchambuzi wa soka kwa kompyuta
Klopp ameongeza kwa kusema kuwa, huvaa nguo inayomfanya ajisikie huru, awe na uwezo wa kuruka hapa na pale.
“ Nina suti nyingi za harusi, misibani kwahiyo hata mtu akiniambia nivae suti wala sio kitu cha ajabu kwangu”
“huwa sipendi kufikiria cha kuvaa kabla ya mchezo, kwahiyo nafurahi klabu inanipa vazi amablo naweza vaa na kufanya kila kitu uwanjani lakini sio suti” aliongezea Klopp.
Liverpool kwa sasa inaongoza ligi ikiwa na
alama 15
baada ya leo kuibuka na ushindi wa goli 3-1 dhidi ya NewCastle United
nyuma ya mahasimu wao Man City wenye alama 10 katika mechi 5 walizocheza.