Baada ya siku za hivi karibuni Mbwana Ally Samatta kuonekana kwenye mitandao yake ya kijamii akiwa Ujerumani.
Kuna tetesi kuwa Mbwana Ally Samatta yuko Ujerumani kukamilisha usajili na moja ya klabu ya ligi kuu nchini Ujerumani, Schalke 04 inasemekana ndiyo klabu ambayo inamwinda.
Tetesi hizi zimekuwa kubwa baada ya leo KRG Genk kumsajili mshambuliaji mpya raia wa Nigeria ambaye inasemekana ndiyo atakayeziba pengo lake.
Akizungumza na mtandao wa Kandanda.co.tz meneja wa Mbwana Ally Samatta, Jamal Kasongo amekataa kuweka wazi kuhusiana na tetesi hizi.
“Dirisha la usajili la Uingereza limefungwa, yamebaki ya nchi zingine, tusubiri kwa kudra za mwenyezi MUNGU tutaona kitakachotokea” alidai Jamal Kasongo