Tumekutafsria hapa kwa mujibu wa video hiyo hapo juu.
Tunacheza dhidi ya Kenya, ni nafasi yetu nzuri. Timu zote mbili zinatokea Afrika Mashariki, na Kenya ni jirani yetu, tupende au tusipende wote tunaongea lugha moja, Kiswahili. Hivyo hakuna kitu cha kuficha kati yetu uwanjani.
Lakini muhimu ni kuona jinsi tunavyoweza kuwaweka pamoja wachezaji wachezaji wetu.
Tuliona katika mechi dhidi ya Senegal kulikuwa na uzembe mwingi, lakini huwezi kuwalaumu kwa hilo sababu hii ni mechi kubwa kwao katika mashindano makubwa.
Kitu muhimu ni kuona vile tunaweza kuwajenga na kuwapa motisha ya kiakili na kimwili kuhusiana na mechi.
Viwango vya wachezaji havina wasiwasi, tuna wachezaji wazuri tu.