Sambaza....

Imeripotiwa kuwa Rais wa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF), Ahmad Ahmad, amekamatwa na mamlaka nchini Ufaransa alikokuwa akihudhuria mkutano mkuu wa Shirikisho la Soka Duniani (Fifa).

Taarifa hizi zimethibitishwa na FIFA, lakini hakuna sababu za wazi za kukamatwa kwake zaidi ya kusema zinahusiana na mamlake yake akiwa rais wa CAF. Fifa haifahamu kwa undani kuhusu uchunguzi au tuhuma hizo ndio maana haijatoa taarifa kamili.

Ahmad Ahmad (Kulia) wakifuatilia mechi ya AFCON U17 viwanja vya Chamazi, Dar es Salaam.

Ahmad Ahmad anahusishwa na mkataba wa CAF na Puma, kampuni ya vifaa vya michezo.

Hivi karibuni pia kulikuwa na tuhuma ambazo katibu mkuu wa CAF aliziwasilisha FIFA zikitaja tuhuma za rushwa za Ahmad Ahmad na malipo kwenda kwa marais wa mashirikisho.

Sambaza....