Sambaza....

Tujadiliane kwa pamoja. Baada ya mchezo kati ya team Samatta na team Kiba, Samatta aliulizwa na mwandishi wa habari wa kituo cha Azam TV kwanini aliamua kuchagua wachezaji wa zamani.

Mbwana Samatta alidai kuwa wachezaji wa kizazi cha zamani walikuwa na vipaji vikubwa kuliko wachezaji wa kizazi hiki.

Kutoka kushoto, Mwinyi Kazimoto, Amri Kiemba na Chuji (Nyuma)

“Wachezaji wa kizazi cha zamani walikuwa na vipaji vikubwa kuliko wachezaji wa kizazi kipya ingawa na mimi ni mchezaji wa kizazi kipya”- alidai Mbwana Samatta.

Wachezaji wa zamani wana vipaji vikubwa kuliko wa sasa- unakubaliana na kauli hii ya Samatta?

Wewe unaonaje kauli hii kama mdau mkubwa wa soka nchini? Unakubaliana nayo au unapingana nayo kwa sababu zipi ?

Sambaza....