Viungo walioitwa na Amunike kwaajili ya kikosi cha awali, Ibrahim Ajib na Jonas Mkude, ni miongoni mwa wachezaji ambao hawakuwepo katika mazoezi ya mwisho ya Taifa Stars katika uwanja wa Taifa.
Hii inatia wasiwasi kuwa wanaweza kuwa wameachwa katika kikosi hiki.
Shomari Kapombe na Kelvin John pia hawakuwepo katika mazoezi haya, Kapombe inaweza kuwa sababu ya majeruhi.
Leo baada ya mazoezi kocha mkuu Emmanuel Amunike atatangaza rasmi habari hizi, tutawaletea.