- Safari ya Yanga, Mikononi mwa Dube
- Simba na Yanga nani anaongoza kuweka mpira kwapani.
- Yanga Waweweseka! Gamondi Nje!
- Fadlu Tunaamini anawapa Ubingwa Wekundu
- Manuel Neuer ana umri sawa na uchambuzi wa soka kwa kompyuta
Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) na kampuni ya ubashiri wa matokeo ya michezo (SportPesa) wamehibitisha kuwa Mabingwa wa Tanzania bara Simba Sport Club ndio watakaocheza na Sevilla ya Uhispania kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Mei 23 mwaka huu.
Katibu mkuu wa TFF Wilfred Kidao amesema awali ilikuwa Simba wacheze na Yanga ili kufahamu nani atacheza na Sevilla lakini baada ya kuangalia mambo kadhaa wamekubaliana na SportPesa kuwa Simba ndio wanaopaswa kucheza na timu hiyo kutoka Uhispania.
“Kila mmoja anajua ratiba yetu ya ligi ilivyobana, hivyo tukaona kuna ugumu kuwa na mechi ya Yanga na Simba, na tunapaswa kumaliza msimu kabla ya mwezi Juni, na changamoto nyingine ilikuwa ni maandalizi ya timu ya Taifa ya Tanzania iliyofuzu michuano ya Mataifa Afrika (AFCON) nchini Misri,”
“Kwa hiyo tuliangalia ni njia gani ambayo tunaweza kufanya tusikose ujio wa klabu ya kubwa kama hiyo lakini vile vile tusihathiri kalenda ya mpira wa miguu ya nchi yetu, kwa hiyo SportPesa wakaona ni muhimu tuweze kupata timu ambayo itacheza na Sevilla na wakatuandikia barua ya kuomba njia ambazo tunaweza tukazitumia kama wasimamizi wa mpira wa miguu,”
“Kwa hiyo tukaangalia mambo mbalimbali, na kwa kuwa ujio wa Sevilla umeletwa na SportPesa kwa hiyo ni vyema mashindano ya SportPesa Cup yakabaki kuwa msingi mkuu wa kupata timu ya Tanzania ambayo itacheza na timu yoyote itakayoalikwa, hivyo kwa maana ya mashindano yaliyofanyika hivi karibuni ni kwamba timu ya Tanzania ambayo ilifanya vizuri kuliko timu zote za Tanzania ni Simba ambayo iliiingia nusu fainali, kwa maana hiyo ni rasmi Simba ndio itacheza na Sevilla,” Kidao amesema.
Kidao ameendelea kusema kwamba ni jambo kubwa kuipokea Sevilla nchini na watanzania kwa ujumla wao wanatakiwa kuonesha ari na morali kubwa wakati ambapo Simba watakuwa uwanjani, lakini pia ni wajibu wa taasisi nyingine kunufaika na ujio huo baada ya ule wa Everton mwaka 2017.
Hii itakuwa ni mara ya pili kwa Sevilla kucheza katika bara la Afrika, ikumbukwe mwaka jana walicheza mchezo wa Super Cup na Barcelona katika Ardhi ya nchini Morocco ambapo walipoteza mchezo huo.