- Safari ya Yanga, Mikononi mwa Dube
- Simba na Yanga nani anaongoza kuweka mpira kwapani.
- Yanga Waweweseka! Gamondi Nje!
- Fadlu Tunaamini anawapa Ubingwa Wekundu
- Manuel Neuer ana umri sawa na uchambuzi wa soka kwa kompyuta
Ghafla kuna kitu nimekikumbuka sana. Zile serekasi za Haji Manara katika kuitetea timu yake anayoipenda ya Simba Sports Club.
Timu ambayo kwake yeye ndiye msemaji wake mkuu. Yani mkuu wa idara ya habari ya Simba ni yeye Haji Manara.
Idara ambayo mara nyingi imemfanya ajenge uadui na watu wengi, pia imemfanya ajenge urafiki mkubwa pia na watu wengi.
Ni idara hii hii ambayo wengi wanamuona Haji Manara kama kiungo bora katika timu ya Simba katika kuleta hamasa.
Yani wachezaji mara nyingi huongezewa hamasa kubwa na Haji Manara kupitia kauli mbalimbali ambazo huwa anazitoa.
Unaweza kuona kama kitu cha kawaida lakini kusimama mbele za watu na kutamka Simba ndiyo timu imara kuzidi zote , jambo hili huwa lina maana kubwa kwa wachezaji.
Kusimama mbele za watu na kusema Simba ndiyo timu yenye thamani kubwa hapa nchini , jambo hili huwa linamaana kubwa kwa wachezaji.
Yani wachezaji hutakiwa kujiona wao wana thamani kubwa sana. Na wanatakiwa kupigana kwa nguvu ili kuonesha thamani yao ndani ya uwanja.
Hivi vyote vinatokana na Haji Manara. Haji Manara ambaye huja na kauli mbiu ambazo mara nyingi huwa zina nguvu kubwa kwa wachezaji.
Unaikumbuka YES WE CAN? Kauli mbiu ambayo ilikuwa na mchango mkubwa kwa Simba kuivusha hatua ya makundi ya klabu bingwa Afrika msimu huu ?
Alipangwa kwenye kundi ambalo lilionekana gumu haswaa, kundi ambalo lilikuwa na wanafainali wa michuano ya vilabu ya CAF msimu jana.
Yani As Vita aliyekuwa mwana fainali wa kombe la shirikisho barani Afrika na Al Ahly aliyekuwa mwana fainali wa kombe la klabu bingwa barani Afrika.
Hili ndilo ƙundi ambalo alikuwepo Simba. Ndilo kundi ambalo wengi hawakumpa nafasi kubwa Simba kupita lakini Haji Manara alikuja na kauli mbiu ya YES WE CAN.
YES WE CAN. Aliwaaminisha mashabiki na wachezaji ƙuwa wanaweza kufanya chochote kikubwa sehemu ambayo wanaonekana kutopewa nafasi ya kufanya hicho kikubwa.
Hata mechi ya mwisho ya kundi ambayo iliwakutanisha na As Vita, Haji Manara alikuja na kauli ya DO or DIE.
Kwa tafasri ya haraka haraka ilikuwa na maana ya kufa na kupona. Hii mechi ilikuwa ya muhimu sana na ilitakiwa wachezaji wapambane ili wapite.
Ndicho kitu kilichotokea , walipambana waliifunga As Vita na kupita kwenda hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa barani Afrika.
Huyu ndiye Haji Manara, mtu pekee ambaye anaaminika kuwa ndiye aliyekuwa chachu kubwa ya mashabiki wa Simba kujaza uwanja katika mechi za nyumbani kwenye michuano ya Ligi ya mabingwa.
Ana mazuri yake mengi tu. Na kuna wakati mwingine hufanya vitu ambavyo kwa wengi huonekana havina maana, na mwisho wa siku huchukiwa kama kichekesho kwa wakati huo.
Unakumbuka tukio la Haji Manara kwenda na TV kwenye mkutano wa waandishi wa habari(press conference?)
Bila shaka unaikumbuka sana hiyo siku au tukio husika. Ila kama hukumbuki ngoja niƙukumbushe kitu kimoja ili twende sawa.
Haji Manara alienda na ile TV kwenye mkutano wa waandishi wa Habari kuwaonesha namna ambavyo Simba ilivyodhurumiwa kimaamuzi ndani ya uwanja.
Lilikuwa tukio la ajabu tena linaonekana la kuchekesha hivi. Wengi hawakumwelewa ikiwemo na mimi binafsi, sikumuelewa kabisa.
Niliona anafanya kitu cha ajabu sana siku ile. Lakini wakati natazama mechi ya jana dhidi ya KMC niliona Haji Manara alikuwa sahihi kabisa.
Maamuzi yalikuwa mabovu, mwamuzi alishindwa kutafsiri sheria 17 za mpira wa miguu. Hakufanya maamuzi ambayo ni sahihi.
Ndipo hapo nikamkumbuka Haji Manara. Kuna wakati mwingine haya madudu wanayotafanya hawa waamuzi wanatakiwa waoneshwe.
Yanatakiwa kuoneshwa wazi ili wao pia wayaone. Wasimwangwe haswaa kuna siku aibu itawavaa na watakuwa makini kutafsiri hizi sheria za mpira wa miguu.