Sambaza....

Baada ya timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” kufuzu michuano ya Mataifa ya Africa tayari TFF imeshaanza maandalizi ili tuwe na ushiriki mzuri katika michuano hiyo baada ya kukosekana kwa miaka 39.

Timu ya Taifa ya Tanzania imepata nafasi ya kucheza mchezo wa Kirafiki na timu ya Taifa ya Misri mchezo utakaopigwa nchini Misri June 13 katika mji wa Bourg Al-Arab.
Misri ndio wenyeji wa mashindando hayo baada ya kuipata nafasi hiyo kutokana na Cameroon kupokwa nafasi hiyo kwa kushindwa kutimiza vigezo vya maandalizi.

Sambaza....