Kikosi cha Simba B (U-20) leo walikua na mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Taifa ya vijana ya Cameroon ya umri chini ya miaka 17 wanaojiandaa na michuano ya Afcon itakayofanyika hapa nchini.
Katika mchezo huo wa kirafiki uliofanyika katika uwanja wa JK Park Kidongo Chekundu ulimalizika kwa sare ya bao moja kwa moja mpaka dakika ya tisini.
Cameroon ndio waliokua wakwanza kupata bao katika kipindi cha kwanza kabla ya vijana wa Simba kusawazisha kipindi cha pili na hivyo kufanya dakika 90 za mchezo kumalizika kwa sare ya bao moja kwa moja.
Timu ya Cameroon tayari imewasili nchini iliwa tayari kabisa kushiriki michuano ya Afcon kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 inayofanyika Tanzania kwa mara ya kwanza.