Hatimaye Ole Gunnar Solskjaer apata mkataba wa kudumu kukinoa kikosi cha Red Devils, Manchester United.
Solskjaer amepewa mkataba wa miaka mitatu baada ya kushinda michezo 14 kati ya 19 aliyoingoza Man U kama kocha wa muda.
Mkataba wa Solskjaer utakuwa unamlipa paundi milioni 7 kwa msimu ikiwa ni chini ya nusu aliyokuwa akilipwa kocha Jose Mourinho ya paundi milioni 18 kwa msimu.
Usizikose hizi pia…
- Safari ya Yanga, Mikononi mwa Dube
- Simba na Yanga nani anaongoza kuweka mpira kwapani.
- Yanga Waweweseka! Gamondi Nje!
- Fadlu Tunaamini anawapa Ubingwa Wekundu
- Manuel Neuer ana umri sawa na uchambuzi wa soka kwa kompyuta
Solskjaer ambaye tayari ameshapendekeza majina ya wachezaji wanaitajika kukisuka kikosi cha Man U na bosi wa klabu hiyo Ed Woodward amemuhakikishia kutenga fungu la kutosha kwa usajili pekee, Solskjaer amepata shavu hilo ambalo kwake yeye lilikuwa kama ndoto aliyokuwa akiiota kila uchao.
Rekodi zake ndani ya klabu hiyo ni nzuri kwani alishawahi kuifungia klabu hiyo magoli 126 katika mechi 366 alizocheza kuanzia mwaka 1996 hadi mwaka 2007.
Pia akiwa kama kocha hadi sasa amesimamia mechi
19, ameshinda 14, sare 2, kupoteza mechi 3, “ cleansheet” michezo 7, asilimia
za ushindi ni 74, magoli ya kufunga 40, wastani wa goli 2.11 kwa kila mchezo na
kufungwa magoli 17 ikiwa ni wastani wa goli 0.89.