Ni nani wa kurejesha tena hamasa hii na morali ya mashabiki wa Mbeya City FC?? Historia iliyoandikwa kwa gharama kubwa imepotea kwa hasara isiyo na kipimo!
Ni vigumu sana kuandika historia ila ni rahisi kuisahau. Hii ndio Mbeya City FC iliyowachukua baadhi ya mashabiki wa Simba na kuwafanya waitwe kizazi kipya, mambo yalipoanza kwenda kombo kwa MCC huku MO kaichukua Simba nao wale wa kizazi kipya wamerudi nyumbani!
Ama kwa hakika watu wa Mbeya tuna hili deni la klabu yetu ya Mbeya City. Sijui ni mashabiki au ni uongozi chini ya Halmashauri ya jiji aliekosea! Kwa hakika kila mmoja anamakosa yake katika hili. TUJIANGALIE UPYA.
Juniour Matukuta.