Sambaza....

Shirikisho la soka barani Afrika limetupilia mbali ombi la Liberia kubadilisha uwanja utakaotumika kwenye mchezo wao wa kuwania nafasi ya kushiriki kwenye michuano ya Mataifa Afrika dhidi ya DR Congo kutokana na tishio la ugonjwa wa Ebola.

Shirikisho la soka nchini Liberia liliandika barua ya maombi ya kubadilisha uwanja kwenda CAF kuomba kubadilisha uwanja uliopo jijini Kinshasa lakini leo barua imejibiwa na kueleza kuwa sehemu ambazo kuna tishio la ugonjwa wa Ebola zipo mbali na jiji hilo hivyo hakutakuwa na mabadiliko yoyote ya uwanja.

“Kwa mujibu wa ripoti, Virusi vinavyosababisha Ebola vipo mbali na mji wa Kinshasa na hivyo hakuna hatari yoyote ya kuandaa mchezo huo, kwenye uwanja uliokuwa tayari umepangwa,” Mkurugenzi wa mashindano wa CAF Samson Adamu amesema.

“CAF itaendelea kuwasiliana na shirika la afya duniani (WHO) kupata taarifa za kina kuhusiana na ugonjwa huo, hata hivyo tunaendelea kufuatilia ili na kuandaa mazingira ya usalama kwa wale wote ambao wanauhisika kwenye mchezo huo,” amesema.

Kutokana na majibu hayo ya CAF, tayari msafara wa awali wa Liberia umeelekea nchini DR Congo kwa ajili ya kuendelea kufanya maandalizi ya mapema kwa ajili ya mchezo huo ambao utafanyika Jumapili.

Sambaza....