Shirikisho la soka barani Afrika CAF limekanusha taarifa zilizokuwa zikizagaa mitandaoni na kwenye vyombo mbalimbali vya habari barani Afrika kuwa rais wa shirikisho hilo Ahmad Ahmad alinyimwa ruhusa kuingia nchini Marekani.
CAF imesema inashangaa kuona taarifa hizo kwani hakukuwa na katazo lolote kwa rais Ahmad na ujumbe wa CAF ambao walipaswa kuwepo nchini Marekani kuhudhuria mkutano wa FIFA unaofanyika leo mjini Miami.
“Tunasema kuwa hakuna katazo lolote kwa CAF na ujumbe wake kuingia nchini Marekani, rais alipewa Visa na ubalozi wa marekani nchini Misri, na anafahamu kwa uzuri taratibu zote za kuomba visa kwa kila nchi,”
“CAF inawaomba wale wote wanaosambaza taarifa hizi za uwongo kuacha mara moja na kuheshimu taaluma ya uandishi wa habari inayokataza kueneza habari za uzushi”