Sambaza....

Kocha wa timu ya Taifa ya Ujerumani Joachim Low ametangaza kuwaacha baadhi ya wachezaji nyota na wakubwa katika kikosi chake kuelekea michuano ya Euro mwa 2020.

Joachim Low ameweka wazi kua wachezaji Thomas Mullar, Jerome Boateng na Math Hummels hawapo katika mipango yake kuelekea michuamo ya Euro mwakani ambayo itachezwa kwa mfumo mpya pia.

Nyota wote hao wanaitumikia klabu kubwa na kongwe nchini Ujerumani ya Fc Bayern Munich. Lakini wachezaji wote hao walikuepo katika kombe la dunia la mwaka 2014 nchini Brazil ambapo Ujerumani waliibuka mabingwa kwa kuifunga Argentina katika fainali.

Michuano hiyo ambayo bingwa mtetezi ni Portugal inatarajiwa kuanza kutimua vumbi June 12 mpaka July 12 katika miji 12 ya nchi 12 tofauti.

Sambaza....