Sambaza....

Kuna kitu unatakiwa kukiangalia kwa makini sana. Hivi ushawahi kujiuliza tangu Juma Kaseja astaafu ni golikipa gani ambaye amesimama kututetea?

Bila shaka utanijibu ni Aishi Manula. Ni ukweli usiopingika kuwa Manula amekuwa ndiye mtu pekee anayetutetea sisi.

Tumempa kila kitu, imani yetu imekuwa kubwa sana kwake. Tumemwamini sana , tukaamini mikono yake iliyokulia Azam Fc.

Mikono yake imekuwa hodari sana kututetea na hatujawahi kabisa kuwa na golikipa mwingine ambaye anayeweza kumpa changamoto Aishi Manula.

Siyo changamoto tu, hata siku ambayo Aishi Manula ataumia ni nani ambaye anayeweza anaweza kuziba pengo lake ?

Hapa ndipo kichwa kinapoweza kuuma. Kuna magolikipa wachache sana ambao wanauwezo unaokaribiana na Aishi Manula.

Beno Kakolanya

Wachache sana, na kwa haraka haraka golikipa pekee ambaye analingana kiwango na Aishi Manula ni Beno Kakolanya.

Huyu anamikono imara sana , ana mikono ambayo inauwezo wa kuilinda bendera ya Tanzania ili isianguke na iendelee kupepea kwenye kila ugumu.

Ni ngumu mno kupata magolikipa bora wanaonafanana kwenye timu , na hii huwa na faida kubwa sana kwenye timu.

Kwanini nasema hivo ?, ngoja nikurudishe nyuma. Unakumbuka hapo nyuma nilipokuambia kuwa Aishi Manula anahitaji mtu wa kumpa changamoto?

Changamoto ni chachu kubwa sana ya mafanikio, hakuna mafanikio yanayokuja bila kuwa na changamoto.

Changamoto huimarisha sana mtu anayekimbilia mafanikio. Changamoto hukomaza sana kila mtu anayetamani kufikia mafanikio makubwa.

Tuna tamani sana kufikia mafanikio makubwa kama nchi, na ili tufikie mafanikio makubwa kama nchi kwenye soka tunahitaji hiki kitu pia pamoja na kuhitaji vitu vingi.

Ndani ya kikosi cha timu ya Taifa kuwe na changamoto kwenye kikosi cha timu ya Taifa. Changamoto ambayo inaweza kumfanya mchezaji apigane ili apate namba.

Kusiwe na wepesi wa kupata mamba ndani ya kikosi. Kuwe na ugumu, yani mtu apate namba kwa jasho haswaaa!.

Jasho ambalo litamwiimarisha mchezaji husika, kiasi kwamba atakapopata namba ndani ya kikosi cha kwanza awe mchezaji imara haswaa!.

Aishi Manula anakosa changamoto ndani ya kikosi cha timu ya Taifa. Na mtu anayeweza kumpa changamoto kubwa ni Beno Kakolanya.

Hiyo ni moja, mbili kuna kitu ambacho huko juu nimekiongea pia. Kuhusu majeraha. Jaribu kujiuliza kama Aishi Manula akaumia ni kipa gani ambaye anaweza kuzipa pengo lake ?

Hapo ni pagumu, hakuna golikipa ambaye anauwezo unaokaribiana na Aishi Manula kama Beno Kakolanya, hakuna raha ya kama kuwa na kikosi kipana.

Tafasri halisi ya kikosi kipana ni hii hapa tu, kikosi kipana ni kuwa na wachezaji wengi ambao wanalingana viwango.

Aishi Manula

Tafasri ya kikosi kipana siyo kuwa na wachezaji wengi tu. Tunatakiwa kuwa na kikosi kipana, kikosi ambacho kitakuwa na wachezaji wanaolingana viwango.

Tunakosa hicho na tunakihitaji hicho kabisa. Lakini tunakipataje?, simpo ni kuwatunza wachezaji bora ambao tunao.

Beno Kakolanya ni mchezaji wetu sisi Watanzania. Watanzania ambao tunataka kuwa na wachezaji wengi bora ndani ya kikosi chetu cha timu ya Taifa.

Tunamwihitaji sana Beno Kakolanya. Tena sana, tunahitaji kumlinda Beno Kakolanya ili aweze kutusaidia sisi Watanzania ambao tunahamu ya kufika sehemu nzuri.

Lakini kwa bahati mbaya Beno Kakolanya kwa sasa anamgogoro na kocha wake wa timu ya Yanga, Mwinyi Zahera.

Mgogoro ambao umemfanya asimamwishwe kucheza ndani ya kikosi cha Yanga kwa muda mrefu. Yuko nje ya uwanja kwa muda mrefu.

Hii siyo hatari kwa Beno Kakolanya pekee , hii ni hatari hata kwetu Watanzania ambao tunandoto ya kuiona timu yetu ya Taifa ikifika mbali.

Hatuwezi kufika mbali bila kuwa na wachezaji wengi bora ndani ya timu yetu ya Taifa. Inawezekana Mwinyi Zahera hajui hilo.

Inawezekana Mwinyi Zahera hajui matamanio yetu , ndiyo maana anazidi kumbania Beno Kakolanya, ugomvi wao sisi nyasi ndiyo tunaoumia.

Sambaza....