Binadamu anajifunza wakati wote kutokana na makosa au kwa uhitaji wa jambo fulani, na mara zote lengo la mtu kukwambia ukweli hata kama unauma ina maana kuwa ubadilike au uboreshe au upunguze, lengo likiwa ni moja tu kukufanya uinuke tena.
Tovuti yetu ya kandanda.co.tz mwishoni mwaka 2018 iliandaaa utaratibu ambao uliwawezesha wasomaji wetu, makocha na waandishi wa habari kuwapigia kura wachezaji na makocha waliopendekezwa na timu yetu. Utaratibu huu tuliupa jina la NANI GALACHA WA KANDANDA 2018. Lengo kuu la utaratibu huu ilikuwa ni kutambua mchango wa wachezaji na makocha ambao wamehusika katika soka la Tanzania kwa mwaka mzima yaani Januari hadi Disemba 2018. Na hakika tumefanikiwa pakubwa sana.
Hata hivyo baada ya maoni kutoka kwa wadau wa soka nchini ikiwemo walimu na watu wa ufundi, pamoja na utafiti wetu, timu ya Kandanda.co.tz chini ya kampuni ya GALACHA, ilikaa chini na kuandaa utaratibu vizuri na vigezo vya kuandaa na kutoa tunzo za GALACHA WA KANDANDA. Vigezo vikuu vinne ambavyo vimeainishwa na pia kuwasilishwa kwa shirikisho kwaajili ya baraka zao ni;
Kwanza, ni kutazama mafanikio ya mchezaji kwa upande wa tuzo mbalimbali alizozikusanya, vikombe , timu yake ya taifa na mafanikio binafsi ndani ya mwaka mzima.
Pili, mchango wake katika mafanikio ya katika klabu na timu yake ya taifa.
Tatu, ni lazima awe anacheza ligi ya Tanzania au Mtanzania anayecheza nje ya nchi.
>>>Vigezo na Nafasi za GALACHA WA KANDANDA
Na mwisho ni lazima awe mchezaji wa klabu au timu ya taifa ya nchi yake kwa muda usiopungua mwaka mmoja yaani kuanzia Januari hadi desemba, kigezo hiki kitatumika kote isipokuwa kwa tuzo maalumu. Soma zaidi hapa…
Ukitazama katika orodha ya awali ya NANI GALACHA WA KANDANDA 2018 kama inavyoonekana katka picha hii chini, wachezaji wawili Ramadhani Kabwili na Heritier Makambo hawakutakiwa kuwemo katika kupigiwa kura kwa mujibu wa vigezo vyetu tajwa. Wachezaji hawa wameanza kuhusika katika ligi kuu mwezi Agosti ambapo ligi ilikuwa ndio inaanza. Kwa kuwa hiI zilikuwa ni kama majaribio na sehemu ya kujifunza tutaonyesha jinsi wachezaji na makocha walivyopata kura zao za Wasomaji wetu na, Waandishi na Makocha.
Matokeo baada ya upigwaji kura wa awali
Katika upigwaji kura wa awali, ilionekana kabisa jinsi waandishi na makocha, walivyotofautiana katika kile wanachokiona kwa namna tofauti. Unaweza kuona katika chati hii katika picha zifuatazo, wachezaji na makocha ambao wangetunukiwa Tunzo za GALACHA WA KANDANDA unaweza kuwaona upande wa duara upande wa kushoto wale wenye asilimia kubwa.
Heritier Makambo alijiunga na Klabu ya Yanga Julai Mosi, 2018, ameitumikia Yanga kwa miezi mitano pekee kabla ya kuisha kwa mwaka 2018, hivyo kwa vigezo ambavyo tumeainisha hakutakiwa kuwa katika orodha ya wachezajji hawa. Kama ingekuwa ndio utoaji tunzo, zingaenda kwa Jonas Mkude.
Kwa lengo la kuboresha zaidi, utaratibu wa TUNZO hizi kama ilivyo fafanuliwa katika muongozo kura ndizo zitakazoamua yupi ni mchezaji bora, kipa bora, kocha bora, mchezaji chipukizi na mchezaji wa Tanzania anayecheza soka la kulipwa nje ya nchi.
Kura hizo ambazo zitapigwa na wadau wa soka nchini kuanzia mashabiki, makocha na waandishi wa habari nchini zitakuwa zinahesabiwa kwa utaratibu maalumu wenye uzito maalumu utakao wezesha kumpata mshindi halali na mwenye sifa yakinifu zinazomfanya awe ndie mtu sahihi.
- Mashabiki watachangia asilimia 20 ya kura za kila kigezo katika kura zilizopigwa kupitia tovuti ya kandanda.co.tz na njia nyingine rasmi.
- Makocha wakuu na manahodha wa timu za ligi kuu Tanzania bara watachangia asilimia 35 ya kura zote.
- Waandishi wa habari kote nchini, wana uzito wa asilimia 45 katika jumla ya kura hizo.
Vigezo hivi ndivyo vilivyotumika pia katika kura hizi za awali na vitaendelea kutumika kwa miaka mingine, na uboreshaji utakuwa ni mkubwa zaidi.
Tazama pia ukurasa wetu wa Tunzo zitakazotolewa na zinazotolewa