Sambaza....

Kocha wa Kariobangi Sharks ya nchini Kenya William Maluya amesema mchezo ambao Yanga walipoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Stand United ndio mchezo pekee ambao waliweza kusoma mbinu zao kabla ya kucheza nao leo.

Maluya amesema hata Yanga walikuwa bora, na pengine bao la mapema ambalo walilipata ndilo liliharibu mipango yao na kuwafanya kukubali kichapo cha mabao 3-2 kutoka kwao.

Kocha wa Kariobangi Sharks William Maluya.

Kariobangi wamekata tiketi ya kucheza nusu fainali baada ya kuwachapa Yanga kwa mabao 3-2 leo kwenye uwanja wa Taifa katika michuano ya SportPesa Cup.

Sambaza....