Sambaza....


MLINZI wa pembeni wa Nkana Red Devils ya Zambia, Hassan Kessy anewapongeza Simba SC kufuzu hatua ya makundi ligi ya mabingwa Afrika, lakini pia amewaonya.

Kessy alikuwa bora kwa dakika zote 180 za mipambano miwili ya hatua ya mtoano kati ya mabingwa wa Tanzania bara Simba dhidi ya ‘ Mashetani Wekundu’ hao wa Zambia licha ya kuondolewa kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-3.

” Tumetolewa katika ligi ya mabingwa lakini bado tupo katika mashindano ya Caf. ” anaanza kusema beki mbili huyo wa timu ya Taifa ya Tanzania.

” Nichukue nafasi hii kuwapongeza Simba kwa kazi waliyofanya ambayo imewawezesha kufuzu kwa hatua ya makundi lakini wanapaswa kuongeza umakini hasa katika beki yao kama wanataka kufanya vizuri zaidi katika hatua hi yo” anasema Kessy .

” Tulifanikiwa kuwabana na tulikaribia kufuzu kwa hatua ya mbele lakini licha ya kutengeneza nafasi nyingi za kufunga tulishindwa kuzitumia na wao walifanikiwa kutumia nafasi chache walizotengeneza na kushinda.”

” Wamefuzu kwa hatua ya makundi ambayo ni ngumu zaidi hivyo wanapaswa kurekebisha baadhi ya makosa yao ili wafanye vizuri. “

Kessy alikuwa tatizo kubwa kwa mlinzi wa kushoto wa Simba, Mohammed Hussein’Zimbwe Jr’ kutokana na mchezo wake wa kupanda mara kwa mara anaamini kikosi chao kinaweza kufanya vizuri katika michuano ya Confederation Cup walipoangukia.

” Tuna timu nzuri na tutaweza kufuzu kwa hatua ya makundi ya michuano ya Shirikisho baada ya kushindwa kufanya hivyo katika ligi ya mabingwa.”

Sambaza....