Klabu ya Real Madrid imethibitisha kuwepo nje kwa takribani wiki nne, sawa na mwezi mmoja kwa mshambuliaji wake, Mhispaniola Marcos Asensio.
Asensio mwenye miaka 22, alipata majeraha ya upaja katika mchezo wa nusu fainali ya klabu bingwa ya dunia siku ya jumatano dhidi ya Kashima Antlers ambapo Real iibamiza Kashima goli 3-1.
Tayari klabu ya Madrid imeshathibitisha kuwa mshambuliaji huyo aliyeifungia timu yake magoli 3 katika mechi 24 msimu huu ataikosa fainali ya klabu bingwa ya dunia dhidi ya Al Aian leo jumamosi.
Katika kipindi chote cha wiki nne, Asensio atazikosa mechi nyingi za ligi zikiwemo dhidi ya Villa Real, Real Sociedad, Real Betis, na Sevilla ambazo zote zitachezwa mapema mwezi januari mwakani.
Pia atazikosa mechi zote mbili dhidi ya Legane
katika kombe la Copa del Rey.