Sambaza....

Mlinda Mlango wa timu ya soka ya AC Milan Gianluigi Donnarumma ameweka rekodi ya aina yake kwa kuwa mchezaji wa kwanza kwenye ligikuu nchini Italy ‘Seria A’ kucheza michezo 100 mfululizo kwa dakika zote 90 akiwa na umri wa miaka 19 pekee.

Donnarumma ameweka rekodi hiyo ya kipekee wakati akiitumikia timu yake ya AC Milan jana dhidi ya Torino na kulazimishwa sare ya 0-0  kwenye uwanja wa Giuseppe Meazza mjini Milan jana.

Mpaka sasa Donnarumma amecheza michezo 125 akiwa na AC Milan na rekodi ya jana inamaanisha kwamba amecheza dakika 900 bila ya kubadilishwa toka alipoingia kama mchezaji wa akiba mwaka 2016 wakati timu yake ilipotoka sare ya0-0 na Chievo Verona.

Aidha katika mchezo huo Donnarumma aliweza kuokoa michomo miwili hatari ya Iago Falque na Andrea Belotti na kuiwezesha timu yake kupata alama moja muhimu nyumbani huku yeye akijitengenezea rekodi hiyo.

Kwa matokeo ya jana, Donnarumma ameisadia timu yake kufikisha alama 26 na kubakia katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi kuu nchini Italy.

Sambaza....