Dakika nane pekee ndizo ambazo ziliwachukua Simba kufunga goli la kwanza kupitia kwa John Raphael Bocco.
Goli hili lilidumu kwa dakika 19 , ambapo Guevand Nzambe aliipatia Mbambane goli la kusawazisha. Goli ambalo liliwapa nguvu Mbambane katika mchezo huu.
John Bocco aliipatia timu yake goli la pili kwa mkwaju wa penalty dakika ya 32. Goli hili lilidumu mpaka dakika ya 83 ambapo Meddie Kagere aliifungia Simba goli la tatu.
Goli hili lilitokana na kipa wa Mbambane kuteleza baada ya kurudishiwa mpira, ndipo hapo Meddie Kagere alipopata nafasi ya kuifungia Simba goli la tatu.
Hassan Dilunga aliyeingia kuchukua nafasi ya John Raphael Bocco alikuwa chachu ya upatikanaji wa goli la nne lilofungwa na kiungo Clatous Chama.
Simba katika mchezo huu ilimtoa Emmanuel Okwi na kumwingiza Shiza Kichuya, baadaye wakaja kumtoa John Bocco ambaye alimpisha Hassan Dilunga, kwa matokeo haya Simba inajitengenezea nafasi nzuri ya kuvuka kwenda hatua ya kwanza ya ligi ya mabingwa barani ulaya