Miaka 14 imepita bila wao kufuzu kucheza mechi za kimataifa. Leo hii Mtibwa Sugar wanaenda kucheza mechi yao ya kimataifa kwa mara ya kwanza baada ya miaka 14.
Mtibwa Sugar wamechagua uwanja wa Chamazi kama uwanja wao wa nyumbani katika mechi hizi za kimataifa.
Na mechi yao ya kwanza itawakutanisha dhidi ya Northern Dyanamo ya Sheli sheli.
Mechi hii inaweza kuonekana nyepesi kwa Mtibwa Sugar kulingana na nchi ambayo timu ya Northern Dyanamo ilipotokea.
Mpira kwa sasa umebadilika, hakuna “under-dog” kwenye mpira wa miguu. Upi ni ubora wa Northern Dyanamo kuelekea mchezo wa leo???
Safu ya Ulinzi.
Timu ya Northern Dyanamo, imecheza mechi 18 mpaka sasa hivi, ikiwa inashika nafasi ya 9 kwenye ligi kuu ya Sheli Sheli.
Katika mechi 18 walizocheza wamefungwa magoli 46 mpaka sasa hivi. Ikiwa ni wastani wa kufungwa magoli 2.5 kwenye kila mchezo.
Kwa hiyo Northern Dyanamo wana safu dhaifu ya Ulinzi ambayo ina nafasi kubwa ya kuruhusu goli kwenye kila mchezo.
Safu ya ushambuliaji.
Katika mechi hizo 18 walizocheza Northern Dyanamo wamefanikiwa kufunga magoli 26 mpaka sasa. Ikiwa ni wastani wa kufunga goli 1.5 kwenye kila mechi.
Kwa hiyo ukitazama wastani wa safu ya Ulinzi na safu ya ushambuliaji, hakuna uwiano mzuri kwenye hii timu. Safu yao Ulinzi inaruhusu sana magoli ukilinganisha na safu ya ushambuliaji inavyofunga.
Safu ya Ulinzi ina wastani wa kufungwa magoli 2.5 , wakati safu ya ushambuliaji ina wastani wa kufunga goli 1.5 kwenye kila mechi. Hata tofauti ya magoli ya kufunga na kufungwa ni kubwa( -26).
Wakati Mtibwa ina wastani mzuri wa magoli ya kufunga na kufungwa ikiwa na wastani wa magoli 6.
Katika mechi hizo 18 walizocheza katika ligi kuu ya Usheli Sheli, Northern. Dyanamo wamefanikiwa kushinda mechi 4, wakatoka sare mechi 3 na kufungwa mechi 11.