Wachezaji watano wa kandanda watakaowania tuzo za mchezaji bora wa Afrika, tuzo ambazo zinatolewa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) wanatarajiwa kutangazwa Jumamosi ya Novemba 17 mwaka huu.
Majina hayo matano yatatangazwa wakati wa kipindi maalumu cha Luninga (BBC African Footballer of the Year programme) mjini Lagos nchini Nigeria ambapo baada ya hapo watafungua njia ya kupiga kura ambapo mashabiki kupitia kwenye mtandao wa www.bbc.com/africanfootball watampigia kura yule wanayedhani amefanya vizuri kwa mwaka husika.
BBC imekuwa na desturi ya kuwapa tuzo wachezaji ambao wanakuwa wamefanya vizuri zaidi kwa mwaka husika ambapo mwaka jana Mohamed Salah aliungana na wasakata kabumbu wengine Afrika kama Riyadh Mahrez, Yaya Toure, Didier Drogba na Jay-Jay Okocha kutwaa tuzo hizo.