Kiungo wa klabu ya Simba, Haruna Niyoñzima, ametemwa rasmi katika kikosi cha timu ya taifa ya Rwanda, baada ya kuitwa kwa miaka 11 mfululizo.
Kikosi cha timu ya Taifa ya Rwanda kinajiandaa na mechi za kufuzu michezo ya Afcon. Kutemwa kwake kumesababishwa na yeye kutopata nafasi ya kucheza katika klabu yake ya Simba kwa muda mrefu.
Hii inaweza ikawa kengele ya hatari kwa Haruna Niyonzima kwa yeye kujituma zaidi ili arudi tena kwenye kiwango chake kilichosababisha aitwe timu ya taifa kwa miaka 11 mfululizo.