Jana beki wa Simba Erasto Nyoni alijumuishwa rasmi katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania “Taifa Stars”. Uteuzi ambao unaonekana kuwa na nguvu katika maeneo yafuatayo.
1: ENEO LA BEKI WA KATI.
Timu ya taifa ya Tanzania ” Taifa Stars” katika mchezo uliopita ilionesha nidhamu mbovu katika eneo la nyuma. Mabeki wake walikuwa wanafanya makosa mengi binafsi ambayo yaliigharimu timu.
Hivo, ongezeko la Erasto Nyoni katika eneo la beki wa kati litakuwa na msaada mkubwa sana kwa sababu litapunguza makosa mengi binafsi ambayo timu ya taifa ilifanya katika mchezo uliopita dhidi ya Cape Verde.
2: KIUNGO WA KATI.
Katika eneo ambalo lilikuwa na udhaifu mkubwa katika mechi iliyopita ni eneo la kiungo. Eneo la kiungo wa kati wa kuzuia ambapo timu ilikuwa inaruhusu sana mashambulizi mengi katika eneo la nyuma. Hivo uwepo wa Erasto Nyoni unaweza ukawa na tiba katika eneo hili kama akipagwa kwenye eneo hili.
3: ONGEZEKO LA WACHEZAJI VIONGOZI.
Erasto Nyoni ni mzoefu na mashindano ya kimataifa, na amekuwa kiongozi katika timu ya Simba. Hivo kuwepo kwake ndani ya kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania “Taifa Stars” kutaongeza idadi ya wachezaji viongozi ambao watakuwa na msaada kuanzia mazoezini, kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na uwanjani.