Sambaza....

Kila kijiwe cha soka kinazungumza mechi ya Simba vs Orlando Pirates na kila ukiona wadau wawili wa tatu wanajadili mambo ya soka basi topic yao kubwa ni mchezo wa Simba na Orlando hapo kesho.

Wapo wadau wengi wasiojua kwamba leo kuna mchezo mkubwa sana pale England wa hatua ya nusu fainali kombe la FA kati ya wenye soka lao la sasa Man City vs Liverpool.

Kila kijiwe gumzo kubwa ni Lunyasi na Pirates mapacha wa nje kwani Simba ana asisiwa 1936 huku mpinzani wake akiasisiswa 1937 kifupi unaweza kusema ni uzao moja na wale wanaopenda kutumia lugha ya kibena tunasema ‘agemate’ wakiwa na maana rika moja.



Wakiwa na wasifu tofauti katika ushiriki wao wa michuano ya CAF iwe kwenye mabingwa au shirikisho lakini wote wawili kama wanahistoria nzuri za kuvutia basi ni siku za nyuma.

Kwa sasa wanakwenda kukutana Estadio de Mkapa hapo kesho panapo majaliwa ya Allah tutakwenda kutizama mechi nzuri yenye kuvutia, atakaye kuwa na ufundi, mbinu bora nidhamu kubwa ya kutimiza hivyo vitu ataibuka na ushindi ikiwemo kuandaliwa vizuri kiakili.

Binafsi naiona mechi kwenye ushindani wa juu sana kwa kuwa mzani “umebalace” hapa hakuna mnyonge wote ni wababe inapokuja swala la kusakata kabumbu uwanjani.

Simba si haba hali kadhalika wageni nao si haba wanaupiga mwingi haswa uliowafanya wakamaliza vinara wa kundi wakiwa na alama 13 miongoni mwa 18 unazopaswa kupata katika makundi kama utashinda zote.


Kwa Simba yeye alimaliza kwenye nafasi ya pili wakiwa na alama 10 nyuma ya RS Berkane katika sehemu ya alama zote 18 katika michezo 6.

Nini maana yangu hapa ili uwe na alama 13 lazima uwe unamatokeo mazuri pia ugenini mfano Orland alishinda nyumbani na ugenini pia pamoja na kulazimisha sare kwenye baadhi ya michezo.



Simba anapaswa kijiandaa vyema kukabiliana na mpinzani wenye sifa ya kushinda au kulazimisha sare ugenini ile imani ya kwa Mkapa hatoki mtu isiwe sababu ya msingi, sababu ya msingi hapa ni ubora wa Simba kwenye ufundi na mbinu ili kupata matokeo bora yatakayomfanya awe amesonga mbele kupitia mchezo wa hapa na kile kitakachofanyika kule ikawe ‘rehearsal’.

Vikosi vyote vina wachezaji wazuri kwa mfano Pirates watakuwa wanajivunia sana Thembankosi Lorch, Terrance Dzvukamanga raia wa Zimbabwe ambaye ni fundi kwelikweli. Mlinzi Paseka Mako na Kwame Peprah wakiunganishwa vyema na kiungo Mndewa Bandile Shandu. kifupi tujiandae kuona marembo kutoka kwa wazee wa “Shibobo”.

Thembankosi Lorch.

Lunyasi kama kawaida yao wakijivuni mtu kama Pape Osman Sakho, Sadio Kanoute Inonga Cris Mugalu Meddie Kagere na Rally Bwalya akichagizwa na uwepo wa Bernard Morrison ambaye atalazimika kutumia nguvu nyingi kwa kuwa mchezo wa pili kule South Africa hata husika nao.

Nachoweza kusema Jogoo awike asiwike kutakucha tuu nasi tutaona mechi bomba sana pale Temeke kwa Mkapa. 

 

Sambaza....