Rais wa Zamalek, Mortada Mansour, ametangaza kujiondoa kwa klabu yake kwenye mechi ya Misri ya Super Cup dhidi ya Al Ahly uliopangwa kuligwa nchini UAE siku chache kabla ya mpambano huo.
The Whites, mabingwa wa ligi msimu uliopita, walitakiwa kumenyana na Al Ahly, mabingwa wa kombe la Misri, Mei 5 katika michuano ya Super Cup ya Misri katika Falme za Kiarabu.
Hata hivyo, kufuatia msururu wa maamuzi ya chama cha soka cha Misri (EFA) kuhusu mshambuliaji wa Al Ahly, Mahmoud kahraba, klabu hiyo iliamua kutojitokeza kwenye mchezo huo. Mwezi uliopita, Kamati ya Nidhamu ya EFA iliamua kutoza faini kubwa ya EGP 1,000,000 kwa Kahraba na kumfungia mechi 12 kwa madai ya kutoa maneno yasiyofaa kuhusu klabu yake ya zamani Zamalek mwezi Januari.
Al Ahly ilikata rufaa dhidi ya marufuku hiyo na Kahraba ameruhusiwa kushiriki michuano ya Super Cup baada ya EFA kuamua tu kuliangalia suala hilo hadi mahakama ya ndani itakapokutana Mei 14.
Tangazo la kujiondoa lilikuja kupitia video ya Mortada Mansour, rais wa klabu hiyo, ambaye alifukuzwa kazi na Wizara ya Vijana na Michezo, kwenye chaneli yake ya YouTube.
“Hatutashiriki mchezo huu baada ya EFA kuamua kuandaa Super Cup na waamuzi wa Misri. Hatutapoteza mchuano mwingine kama fainali ya Kombe la Mpira wa Kikapu la Misri,” Mortada Mansour alisema.
“Suala lilianza pale Zamalek waliponyimwa kusajili wachezaji wapya isivyo haki, na si kwa sababu ya adhabu ya Kahraba hapo awali,” alisema na kuongeza “Ninaomba radhi kwa mashabiki ambao walikuwa wamekata tikiti za Super Cup, Zamalek wako tayari kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya mabingwa wa Ligi ya UAE katika tarehe hiyo hiyo Ikiwa wataalikwa.”
EFA imethibitisha kuwa wanasubiri barua rasmi kutoka kwa Zamalek kuhusu uamuzi wao, na ikiwa imethibitishwa klabu tofauti itachukua nafasi yao. Washindi wa pili wa Ligi Kuu na Kombe la Misri, Pyramids FC wamepewa kipaumbele kuchukua nafasi ya Zamalek, ikifuatiwa na Tala’a El-Gaish iliyoshika nafasi ya nne msimu uliopita ama Future FC.