Kulikuwa na taarifa nyingi hivi karibuni kuhusiana na kambi ya Yanga mkoani Morogoro, ikihusisha uwezekano mkubwa wa Mwinyi Zahera, kocha mkuu wa timu hiyo kutojiunga na timu hiyo ya Wananchi.
Kandanda ilifanya mawasiliano ya moja kwa moja na Zahera kuondoa wasiwasi ambao umetanda kwa mashabiki wa Yanga nchini hapo kabla. Ikiwa leo pia ameshatinga kambimbi mjini Morogoro.
“Ingekuwa kama mimi sirudi, mimi mwenyewe ningesema.” Zahera alianza kwa kusema hivi.
-Mwinyi Zahera (Katikati)
Mitandao ya kijamii iliripoti tetesi kuwa Mwinyi Zahera hatarudi kutokana na kuidai klabu ya Yanga pesa na posho alizokuwa akizitoa kwa timu hio kama msaada.
“Mambo ya maisha yangu ina ishu mia, mshahara sio kitu inanipatia namna ya kuishi. Natumikisha watu 42 huko Congo, watu wanne Ulaya. Sina ulazima wa kufundisha timu yoyote duniani kwaajili ya mimi kuishi. Naweza fundisha timu yoyote duniani miaka hata mitatu bila kulipwa, sasa wale wanaosema mambo hayo (ya kutokurudi Yanga) ni wapumbafu, sababu hawajui namna gani mimi naishi” Zahera Mwinyi.
Zahera alikuwa na likizo ya siku 15, akisisitiza kuwa alifanya ligi mda mrefu bila kupumzika. “Mimi nilifika Ufaransa tarehe 13, na nilisema napaswa kupumzika kwa siku 15. Sababu nilifanya ligi bila mimi kupumzika. Na hivyo nilisema naenda Ulaya kupumzika siku 15”
Kuhusu kulipa timu “Watu wanasema Uwongo, mimi sikuilipia kambi ya timu wala safari yoyote ile”
Yanga imeweka kambi Morogoro, ikijiandaa na mechi za Ligi kuu na Mabingwa wa Afrika, pamoja na maandalizi ya Wiki ya Mwananchi ambalo linalenga kuitaambulisha timu kwa wananchi. Zahera alikuwa na kikosi cha DR Congo katika michuano ya AFCON nchini Misri ambayo imemalizika kwa Algeria kuibuka washindi.