Sambaza....

Kocha mkuu wa Yanga, Mkongoman Mwinyi Zahera amewaomba mashabiki wa timu hiyo kuwa watulivu na kutosikiliza maneno ya mtaani yanayosema kwamba ameikacha timu hiyo na kurejea nyumbani kwao.

Zahera amesema ni kweli anaondoka nchini na anaelekea nchini Ufaransa ambapo atakuwepo huko kwa ajili ya kufuatilia biashara zake na amepanga kurejea nchini Disemba 26 ili kuendelea kukinoa kikosi cha Mabingwa hao wa mara 27 wa Tanzania Bara.

“Nasafiri leo, nitarudi tarehe 26, nitaondoka Ufaransa tarehe 25 na nitafika hapa asubuhi tarehe 26, naenda huko kwa kuna karatasi za kusaini, ni kutokana na mambo yangu ya biashara ya Ulaya, nikishamaliza narudi hapa,

“Wote wale wanaosema mambo ya uwongo eti kocha anaenda ….. kocha anaenda, sio kweli…. Mimi mwenyewe nafundisha wachezaji wangu kuvumiliana na matatizo ndo mimi leo nisema naenda ni uwongo…….ni uwongo,” amesema.

Zahera ameiongoza Yanga katika michezo 16 ya ligi akishinda michezo 14 kati ya hiyo, matokeo ambayo yanamfanya kukaa kileleni  akiwa na alama 44.

Sambaza....