Mkurugenzi wa wanachama wa klabu ya Yanga CPA Haji Mfikirwa amesema kuwa mpka sasa kuna jumla ya tiketi 18,213 kutoka kwa viongozi na wadau mbalimbali ambao wameshatoa na kuahidi tiketi hizo.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga, Jangwani Haji amesema kuwa ili uweze kupata tiketi unahitaji kuwa na N-card ambayo gharama yake ni 1,000 na gharama ya tiketi ni 5,000.
Mgao wa tiketi utaenda kwa watu ambao watafika uwanjani pekee, hivyo tiketi zitagawiwa kwa makundi yote ya Wananchama kutoka mikoa yote Tanzania na sio Dar Es Salaam pekee yake.
“Watakaopewa tiketi lazima wawe wanaingia uwanjani, hatutagawa tiketi tu kwa kila mtu halafu asije uwanjani,” alisema Haji nakuongeza “Tunaendelea kukaribisha makampuni yaendelee kununua tiketi hizi na sisi kama viongozi tunakuja na utaratibu mzuri wa kugawa hizi tiketi.”
“Lakini kwasasa zoezi la kugawa tiketi limesimama na tutakuja na utaratibu mzuri zaidi ili kila atakepewatiketi aje na aingie uwanjani,” alimalizia Haji.
Yanga itashuka dimba la Benjamin Mkapa saa kumi jioni, jumapili katika mchezo wa kihistoria wa fainali ya kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Algier kutoka nchini Algeria.