Shirikiho la soka Tanzania (TFF ) kupitia kwa katibu mkuu Wilfred Kidao limeiandikia barua klabu ya Yanga kuitaka kubadili jina lake la usajili kutoka “Young African Sports Club” na kuwa “Young African Football Club”. Barua hiyo imedai kuwa, kujiita sports club maana yake ni kujihusisha na michezo mingine tofauti na soka.
TFF imeitaka klabu ya Yanga kufanya hivyo haraka iwezekanavyo kwani ni maagizo kutoka kwa shirikisho la soka duniani (FIFA).
Ikumbukwe kuwa tangu kuanzishwa kwa klabu ya Yanga mwaka 1935, imekuwa ikijulikana kama Young African Football Club, na wengi waliamini kuwa, kuitwa jina hilo ni kutokana na Klabu hiyo kujihusisha na aina moja ya mchezo yaani mpira wa miguu, lakini hivi karibuni Yanga imeonekana kujihusisha na soka la wanawake na hata kuipandisha daraja timu ya wanawake ya Young Princess.
Lakini hii haikutosha kwa klabu hiyo kujiita SPORTS CLUB na badala yake klabu hiyo itaendelea kujulikana kama FOOTBALL CLUB.
Tovuti ya Kandanda imefanya juhudi kubwa za kumtafua afisa habari wa klabu ya Yanga, Dismas Ten, (mbae wakati tukiripoti hii alikuwa safarini Bukoba) ili kujua kujua mchakato wa kubadili jina la klabu hiyo umefikia wapi au wamejipangaje, lakini juhudi hizo ziligonga mwamba, juhudi za ziada zinaendelea kufanywa na tovuti hii ili kupatamajibu kamili.
Imeandaliwa na Sekwao Mwendi