Sambaza....

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania ambaye aliyeipeleka Taifa Stars kwenye michuano ya CHAN, michuano ambayo inahusisha wachezaji wa timu za Taifa wanaocheza ligi ya ndani  Ditram Nchimbi amesajiliwa na Yanga.

Yanga wamekubali kulipa kiasi cha milioni 20 kwa klabu ya Azam FC , mchezaji huyo alikuwa mchezaji wa Azam FC ambaye alikuwa kwa mkopo kwenye klabu ya Polisi Tanzania.

Yanga wameshaachana na washambuliaji wao ambao waliwasajili msimu huu kama Sadney na Juma Balinya , kwa hiyo ujio wa Ditram Nchimbi ni kuja kuchukua nafasi ambazo ziliachwa wazi na washambuliaji hao.

 

Sambaza....