Baada ya Yanga sc kupata sare ya bao moja kwa moja dhidi ya JKT Tanzania katika uwanja wa Jamuhuri Dodoma huku mchezo huo ukishuhudiwa na vurugu kubwa klabu ya Yanga kupitia kaimu katibu wakw imetangaza kuchukua hatua na mlinzi wake wa kati Lamine Moro.
Yanga imetoa barua ikionyesha kusikitishwa na kukerwa na kitendo cha mlinzi wake kutoka Ghana Lamine Moro na kuamua kumchukulia hatua. Yanga imemkata Lamine Moro mshahara wake wa mwezi kiasi cha shilingi 1,000,000/=.
Barua rasmi kutoka ofisi ya katibu mkuu wa Yanga sc ikionyesha hatua waliyoichukua Yanga kwa Lamine Moro.
Katika mchezo huo baada ya kutokea purukushani kati ya wachezaji wa JKT Tanzania na Yanga sc Lamine Moro alionekana kumrukia teke kwa nyuma kiungo mkongwe Mwinyi Kazimoto Mwitula na kupelekea ugomvi mkubwa hivyo wawili hao kuonyeshwa kadi nyekundu.