Simba SC, ndio mabingwa wapya wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara, mara baada ya waliokuwa mabingwa watetezi Yanga SC, kulivua rasmi taji hilo jioni ya leo kwa kukubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Tanzania Prisons mchezo uliopigwa kunako dimba la Sokoine mjini Mbeya
Simba SC, wenye alama 65, hadi sasa zinawafanya kuwa mabingwa, kwa maana Yanga wenye alama 48, baada kucheza michezo 25, hata wakishinda michezo yao yote iliyobakia watafikisha alama 63, tu
Katika mchezo wa leo, mabao ya Prisons yalifungwa na Eliuter Mpepo kwa njia ya penati dakika ya 57, kufuatia Thaban Kamusoko wa Yanga kuushika mpira ndani ya eneo la penati
Salum Bosco, aliipatia Prisons bao la pili kunako dakika ya 84, akitumia vema makosa ya walinzi wa Yanga
Kwa matokeo hayo, yanaashiria kuwa Yanga SC, hawatoshiriki michuano ya Afrika mwakani kufutia pia kutolewa kunako michuano ya kombe la Shirikisho la soka nchini TFF (Azam Sports Federation Cup)
Tanzania Prisons iliwakilishwa na. Aaron Kalambo, Michael Ismaily, Laulian Mpalile, Nurdin Chona, James Mwasote/ Vedastus Mwahiambi dk 62, Jumanne Elfadhil, Benjamin Asukile, Cleophace Mwandala/ Adam Kimbongwe, Mohammed Rashid, Ramadhan Ibata/ Salum Bosco dk 80, na Eliuta Mpepo
Yanga SC. Benno Kakolanya, Juma Abdul Jaffar, Emmanuel Martin, Pato Ngonyani, Abdallah Shaibu, Makka Edward, Paulo Godfrey/ Amis Joselyn Tambwe dk 82, Thaban Kamusoko, Matheo Anthony, Yohana Nkomola, Baruani Akilimali/ Yusuph Suleiman dk 81