Sambaza....

Uongozi wa klabu ya Lipuli FC, ya Iringa, umewajibu viongozi wa Yanga kuhusiana na barua yao yenye ombi la kupatiwa mshambuliaji Adam Salamba ili akaisaidie timu yao katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika

Ikumbukwe kuwa Yanga SC, walituma barua kwa uongozi wa Lipuli wakiomba wapatiwe mshambuliaji Adam Salamba, ili aongeze nguvu katika mashindano ya kimataifa kutokana na baadhi ya wachezaji wao hasa katika safu ya ushambuliaji kuwa majeruhi

Kwa mujibu wa barua ya kutoka uongozi wa Lipuli kwenda Yanga, imeeleza kuwa baada ya kikao cha Kamati ya utendaji ya klabu hiyo kulijadiri suala hilo umefikia mamuzi ya kutowapatia Yanga mchezaji huyo

Aidha barua hiyo ya kuwajibu Yanga iliyosainiwa na Katibu wa klabu hiyo, Amos Erias Lweramila, imefafanua kuwa hawawezi kumruhusu Salamba kwa sababu kanuni za CAF, FIFA na TFF haziruhusu mchezaji mmoja kuchezea klabu zaidi mbili kwa msimu mmoja

Uongozi wa Lipuli FC, umewashauri Yanga kutafuta mchezaji mwingine kwa manufaa ya klabu yao

Sambaza....