Sambaza....

Yanga wanatarajia kuondoka nchin kesho alfajiri kuelekea nchini Nigeria katika mchezo wa kwanza wa robo fainali dhidi ya Rivers United lakini tayari wameshataja viingilio vitakavyotumika kwenye mchezo wa marudiano April 30.

Ikiwa tayari kwa safari ya Nigeria Alli Kamwe msemaji wa klabu ya Yanga amesema wanatangaza viingilio vya mchezo wa marudiano dhidi ya Rivers utakaofanyika katika Dimba la Benjamin Mkapa April 30 mwaka huu.

Alli Kamwe “Tayari tiketi zimeshaanza kuuzwa kuelekea mchezo huo wa marudiano. Viingilio vitakua ni VIP A 30,000, VIP B 20,000 na viti vya rangi ya machungwa ni 10,000 tu wakati kule mzunguko itakua ni 5,000 tu.”

Msemaji wa Klabu ya Yanga Alli Kamwe akiongea na Waandishi wa Habari za Michezo makao makuu ya klabu ya Yanga.

Msemaji wa huyo wa Yanga amesema wametangaza viingilio mapema ili watu wanunue tiketi mapema na kuweza kuujaza uwanja kwenda kuwapa sapoti wachezaji wao katika kwenda kuandika historia mpya.

Watanzania pia aliwaasa kuwaonyesha watu ukubwa wao na kuoonyesha kwanini hii ni ligi bora namba tano Afrika kwakununua tiketi mapema huku akitoka mfano wa mashabiki wa Al Ahly waliomaliza tiketi ndani ya masaa 24 tu kuelekea mchezo wao dhidi ya Al Hilal.

“Watanzania tunajisifia sana sisi ni mashabiki bora na tunaupenda sana mpira, tuonyeshe sasa kwa vitendo kwa kununua tiketi mapema ili tufike huko juu kwa wenzetu wenye ubora wenye ubora kuliko sisi,” alisema na kuongeza

Mashabiki wa Klabu ya Yanga.

Tununue tiketi ili tuwape motisha wachezaji wetu na tuwasaidie kuweka rekodi yakwenda nusu fainali ya Shirikisho Afrika hiki ndio kizazi cha dhahabu chetu Wananchi. Tiketi tumeanza kuziuza leo mimi kama Afisa habari nitajivunia sana kama siku mbili kabla ya mchezo ziishe zote ama angalau hata nusu,” alimalizia Alli Kamwe.

Katika hatua nyingine Yanga wamepunguza bei ya jezi zao za Kimataifa kutoka 50,000 na sasa zitapatikana kwa 40,000 pekee katika duka la Klabu pale Jangwani makao makuu ya Yanga.

Alli Kamwe “Tumeshusha bei ya jezi kutoka 50,000 mpaka 40,000 kwa sababu kuu mbili, kwanza kutoa zawadi ya Eid lakini pia sababu nyingine ni mchezo wa pili tunataka kila mtu aje uwanjani na jezi ya Kimataifa katika mchezo wa marudiano.”

Yanga watashuka Dimbani Jumapili ijayo ya April 30 katika Dimba la Benjamin Mkapa katika mchezo wa marudiano ambapo kama watapata matokeo mazuri kwa michezo yote miwilo basi watasonga mbele na kwenda nusu fainali.

Sambaza....