Ligi kuu Tanzania bara imeendelea jana katika miji tofauti ya Tanzania , macho ya watu wengi ambao ni wapenzi wa mpira wa miguu hapa Tanzania yalikuwa kwenye viwanja vya mikoa miwili.
Mkoa wa kwanza ulikuwa Dar es Salaam ambapo Kuna uwanja wa Benjamini William Mkapa, na mkoa wa pili ni Mara ambako kuna uwanja wa kumbukumbu ya Karume pale mjini Musoma.
Miji hii miwili ilikuwa imebeba timu mbili ambazo zinashindana kupata nafasi ya pili katika msimamo wa ligi kuu Tanzania bara. Yanga ambayo ina alama 60 na Azam FC yenye alama 59 Ndiyo timu ambazo zinapigana kugombani nafasi ya pili.
Akizungumza na mtandao huu wa kandanda.co.tz kuhusu uwezekano wa Azam FC wa kushika nafasi ya pili kwenye ligi kuu Tanzania bara , Afisa habari wa Azam FC amedai kuwa kwao nafasi ya pili ni yao kwa sababu Yanga wanabahatisha.
“Nafasi ya pili kwetu hatuwezi kutumia nguvu kwa sababu hii ni nafasi yetu na hao wanaoshikiria kwa sasa hawana uwezo wa kufanya chochote kwa sababu wanabahatisha sana , tunajua huko wanakoenda wataanguka tu”- alisema Afisa habari huyo wa Azam Fc