Sambaza....

 

Jana mtandao wa kandanda.co.tz ulikuwa na Mwinyi Zahera maeneo ya mlimani city kwa ajili ya mahojiano maalumu.

Kwenye mahojiano hayo kocha huyo wa zamani wa Yanga aliulizwa maswali mengi na mtandao huu , Lakini moja ya swali ambalo aliulizwa na kuachwa kwa wachezaji aliowasajili .

Moja ya wachezaji ambao walisajiliwa na Mwinyi Zahera ni Juma Balinya ambaye alisajiliwa na Mwinyi Zahera Lakini kwenye dirisha dogo la usajili aliachwa.

Alipoulizwa anajisikiaje kuona baadhi ya wachezaji aliowasajili wameachwa kwenye dirisha dogo baada ya yeye kuondoka tu kwenye klabu hiyo.

Zahera Mwinyi

Kocha huyo alisema Yanga walifanya kosa kumuacha Juma Balinya kwa sababu ni mchezaji mzuri ambaye angewasaidia sana Yanga.

“Juma Balinya ni mchezaji mzuri , tulimsajili kwa sababu alikuwa na takwimu nzuri sehemu aliyokuwa anatoka na tulijua huyu ni mshambuliaji mzuri “-alisema kocha huyo.

Balinya (Kulia)

Pia Mwinyi Zahera alidai kuwa Yanga walitakiwa kumpa muda Mwinyi Zahera na angewasaidia kipindi hiki timu yao inapohangaika na kufunga.

“Yanga kwa sasa wanahangaika sana kufunga , safu yao ya ushambuliaji ni butu . Juma Balinya muda huu angekuwa msaada mkubwa sana kwa klabu hiyo ya Yanga”- alisema Kocha huyo.

Mgahawa Cafe & Restaurant ni mdhamini wa Galacha wa Mabao wa Kandanda

Kocha huyo pia aliongezea kuwa Juma Balinya kwa sasa anafanya vizuri na Gor Mahia na anafunga vizuri tu akiwa huko , hayo magoli yangekuwa ya Yanga.

“Kasajiliwa na timu kubwa ya Gormahia , na anafunga magoli tu akiwa na Gormahia. Kwa hiyo hakuwa mchezaji mbaya , mchezaji mbaya hasajiliwi na timu kubwa kama Gormahia na mchezaji mbaya hawezi akawa anafunga tu”- alimalizia kocha huyo wa zamani wa Yanga

Sambaza....