Klabu ya Yanga kupitia makamu mwenyekiti wake, Bwana Mwakalebela wametangaza rasmi kuigomea rangi ya nyekundu ya mdhamini mkuu wa Ligi Kuu Tanzania bara, Vodacom.
Ikumbukwe Vodacom iliingia mkataba na TFF katika kudhamini ligi kuu Tanzania bara kwa miaka mitatu. Mkataba huo unaifaidisha TFF kiasi cha Bilioni 9 ndani ya miaka mitatu.
Katika maelezo yake Mwakalebela, amesema Yanga inatumia rangi tatu tu Kijani, Njano na Nyeusi tu. Hawakotayari kuongezewa rangi nyingine katika jezi zao hata kama wanamatatizo ya kiuchumi. Katiba ya Yanga hairuhusu uvaaji wa rangi nyekundu.
Hivi karibuni GSM pia ilimbidi abadili rangi ya nembo yake ambayo imo katika jezi za Yanga.
Swali la kujiuliza: Ni rangi ipi inawakilisha klabu… Rangi ya Mdhamini au Rangi ya Klabu?