Kuelekea kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu Bara tayari tambo zimeanza kila upande haswa vilabu vitatu vikubwa nchini Simbasc, Yanga na Azam fc vikijinasibu kuutaka ubingwa wa Ligi Kuu Bara.
Akiongea na kituo cha East Afrika Redio katika kipindi cha michezo leo, naibu katibu mkuu Simon Patrick ameweka bayana wanayataka makombe yote ya ndani msimu huu watakayoshiriki.
Simon Patrick “Tumeshamwambia mwalimu malengo yetu tunataka ubingwa msimu huu, kwa kutumia report ya mwalimu aliepita tumesajili vizuri na tumeleta wachezaji wazuri. Na ndio maana tumemleta kocha mzoefu mwenye CV kubwa Afrika.
Tunavitaka vikombe vyote vya ndani msimu huu, sisi tumempa mahitaji yetu na yeye atupe mpango wake tutampa kila kitu atakachotaka mwalimu na ndio maana hata kambi tumehama, alisema anataka sehemu yenye utulivu tukahama pale.”
Kiongozi huyo pia ametanabaisha pia kama atashindwa kufikia malengo wataangalia pia ameshindwaje kufikia malengo.
“Endapo hatofikia malengo na kushindwa tutaangalia ameshindwaje, tumempa mkataba wa miaka miwili lakini tutaangalia kwanza mwaka wa kwanza utakwendaje.” Alimazilia wakili msomi Simon Patrick.
Benchi la ufundi la Yanga linaongozwa na kocha mkuu Zlatiko akiwa na makocha wasaidizi Juma Mwambusi na Said Maulid, kocha wa makipa Vladmir Niyonkuru chini ya meneja Hafidh Saleh.